Kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na China ni chaguo sahihi lililofanywa na Nauru
2024-01-18 10:01:52| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema Nauru kutambua kanuni ya China moja, kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan na kutafuta kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na China ni uamuzi wa pamoja wa baraza la mawaziri la Nauru na ni chaguo sahihi lililofanywa na Nauru kama nchi huru.

Bi. Mao amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari akizungumzia kuhusu Nauru kuvunja kwa ghafla uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan.

Bi. Mao amedokeza kuwa Jumanne bunge la Nauru lilipitisha azimio kwa kauli moja, kuunga mkono na kuthibitisha uamuzi wa serikali ya Nauru wa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na China, kwa mara nyingine tena inaonyesha kwamba kanuni ya China moja ni mwelekeo wa maoni ya jumuiya ya kimataifa.