Mkurugenzi mkuu wa IMF asema ongezeko la pato la taifa la China ni “habari nzuri” kwa dunia
2024-01-18 10:00:22| CRI

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bibi Kristalina Georgieva alipohojiwa kando ya mkutano wa 54 wa mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani huko Davos, amesema ongezeko la uchumi wa China katika mwaka 2023 ni habari nzuri kwa China na nchi nyingine.

Amesema uchumi wa China umetimiza lengo lake la ongezeko la takriban asilimia 5, na hali halisi imezidi lengo hilo, hali ambayo ni habari nzuri kwa China, Asia na dunia nzima, kwani China imetimiza theluthi moja ya ongezeko la dunia. Ameongeza kuwa serikali ya China inadhamiria ongezeko la uchumi lililo bora, na kubadilisha mtindo wa ongezeko kuwa matumizi kutoka uuzaji nje wa bidhaa.

Idara ya takwimu ya China Jumatano ilitangaza kuwa pato la taifa la China la mwaka 2023 limeongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita, na thamani yake inafikia yuan trilioni 126.06 (sawa na dola takriban trilioni 17.71 za kimarekani).