Uganda yasema mkutano wa kikanda kuhusu Sudan uendelee licha ya maandamano
2024-01-18 10:03:39| CRI

Uganda imesema mkutano ujao wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la nchi za Afrika Mashariki (IGAD) unaotarajiwa kujadili mgororo wa Sudan na suala la ufikiaji wa bahari la Ethiopia na Somalia utafanyika leo licha ya maandamano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Bwana Okello Oryem, amewaambia wanahabari mjini Kampala kuwa viongozi wa kanda hiyo watakutana kujadili njia za kutatua mgogoro wa Sudan licha ya serikali ya Sudan kusema haitahudhuria mkutano huo.

Januari 13 Sudan ilikataa kuhudhuria mkutano huo, ikisema hakuna haja ya kufanya mkutano mpya kujadili suala la Sudan kabla ya matokeo ya mkutano uliopita kutekelezwa. Sudan pia iligoma kuwasiliana na IGAD kuhusu kusuluhisha mgogoro huo, ikisema haikushirikishwa kabla ya kuweka suala hilo kwenye ajenda ya mkutano wa Kampala wa IGAD.