China imetoa msaada wa dawa na vifaa vya huduma za afya kwa hospitali kuu ya rufaa ya Sudan Kusini.
Kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada huo iliyofanyika Juba, mkurugenzi mkuu wa huduma za matibabu katika Wizara ya Afya Bi. Harriet Pasquale amesema vifaa hivyo ni muhimu kwa hospitali hiyo inayopokea idadi kubwa ya watu, na moja ya changamoto inayokabiliana nayo ni kuhakikisha vifaa vya matibabu na kudumisha huduma za kawaida hospitali.
Dawa na vifaa hivyo vinashughulikia zaidi ya aina 300 za dawa za kimsingi zinazotumiwa sana katika idara tofauti. Msaada huo wenye jumla ya masanduku 180 na yenye thamani ya dola za kimarekani laki 1.82, pia unajumuisha vifaa vya matumizi ya kila siku ya chumba cha upasuaji na, magonjwa ya wanawake na uzazi, na idara za upasuaji wa jumla.