Watu 9 wauawa katika mashambulio katikati ya Nigeria
2024-01-19 10:35:00| cri

Watu 9 wameuawa katikati ya Nigeria, ikiwa ni wiki chache baada ya kuzuka kwa mashambulio ya kikabila yaliyosababisha vifo vya watu karibu 200.

Maofisa wa mkoa wa Plateau wamesema, watu 9 wameuawa katika mashambulio yaliyotokea jumanne na jumatano katika wilaya ya Bokkos mkoani humo.

Mwenyekiti wa wilaya ya Bokkos Monday Kassah amesema, watu watano waliuawa wakati wakivuna viazi shambani mwao katika eneo la Butura Kampani, na wengine watatu pia waliuawa katika shamba lao la viazi siku ya jumatano.

Mkoa wa Plateau umeshuhudia mapigano ya mara kwa mara ya kikabila na kidini.