Idadi ya watalii wa kimataifa walioitembelea Kenya yafikia milioni 1.75 katika mwaka 2023
2024-01-19 09:31:53| CRI

Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya Kenya imesema idadi ya watalii wa kimataifa walioitembelea Kenya mwaka 2023 inafikia milioni 1.75, ambayo imeongezeka ikilinganishwa na milioni 1.48 ya mwaka 2022.

Wizara hiyo imesema mapato ya sekta hiyo ya mwaka 2023 yameongezeka hadi kufikia dola takriban bilioni 2.06 za kimarekani ikilinganishwa na dola bilioni 1.66 za kimarekani ya mwaka 2022. Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa mjini Nairobi, imesema wizara hiyo inadhamiria kuifanya idadi ya watalii wa kimataifa wanaoitembelea Kenya iongezeke kwa watalii laki 8.25 kila mwaka.