Msukosuko wa kibinadamu barani Afrika una hatari ya kuongezeka kutokana na vita za wenyewe kwa wenyewe, mabadiliko ya tabia nchi
2024-01-19 09:37:02| CRI

Shirika la kimataifa la kutoa misaada (IRC) limesema msukosuko wa kibinadamu unaoziathiri nchi kadhaa za Afrika, hauwezi kupungua wakati majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na migogoro ya kivita inaongezeka katika bara hilo.

Mkurugenzi anayeshughulikia misukosuko ya kimataifa wa IRC Bw. George Readings, amesema Afrika inaendelea kuwa kiini cha msukosuko wa mabadiliko ya tabia nchi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vinazidisha hali duni, kuvuruga maisha ya raia na kuchochea umaskini.

Wakati huo huo Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa mataifa OCHA, imesema zaidi ya watu laki 3.5 kati ya watu milioni 1.8 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanahitaji msaada wa haraka wa kuokoa maisha.