Mpango wa Kimkakati wa “3820”
2024-01-21 15:44:09| CRI

Mwaka 1993, Xi Jinping alipokuwa katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Fuzhou alisema kuwa “Mchakato wa Fuzhou wa kupiga hatua kuelekea karne mpya lazima uwe na nadharia ya kimkakati ya muda mrefu, ambayo inategemea sayansi na kulingana na ukweli halisi, ili mageuzi ya mji huo yaendelezwe vizuri.” Yeye binafsi aliongoza utungaji wa Mpango wa Kimkakati wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya Fuzhou ya miaka 20, ambao uliweka malengo, hatua, mpangilio na kazi kuu za maendeleo ya mji huo za miaka mitatu, minane na 20, ambao ni mpango na mkakati wa jumla wa maendeleo ya mji huo. Hivi sasa nadharia ya mpango wa kimkakati wa “3820” bado ina umuhimu muhimu wa maelekezo. 

Miaka 30 iliyopita, mji wa Fuzhou ulikuwa na msingi dhaifu wa viwanda, kipato cha chini na hali mbaya ya usafiri. Mwezi Aprili mwaka 1990 Xi Jinping aliposhika wadhifa wa katibu wa Chama katika mji huo, alianza kufikiria njia ya ufumbuzi.

Utekelezaji wa mambo muhimu hutegemea mpango mzuri, si kama tu mpango wa muda mfupi wa miaka mitatu na mitano tu, bali pia unahitaji mpango wa muda mrefu wa miaka 20.

Jinsi gani ya kuweka mpango wa maendeleo wa miaka 20? Xi Jinping alitoa maoni ya kufanya uchunguzi na utafiti, na kuanzisha kazi ya kukusanya maoni ya watu, kufanya uchunguzi na utafiti na kujadiliana. Baada ya juhudi za nusu mwaka na kufanyiwa marekebisho mara kadhaa, mwezi Novemba mwaka 1992, “Mpango wa Kimkakati wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii wa Miaka 20 wa Mji wa Fuzhou” ulijadiliwa na kupitishwa katika Mkutano wa Sita wa Kamati ya Chama ya Mji wa Fuzhou.

Lengo la mpango huo ni kuhimiza ukuaji wa uchumi kupanda ngazi kubwa ndani ya miaka mitatu, viashiria vikuu kufikia kiwango cha maendeleo ya miji mikubwa nchini ndani ya miaka minane, na kukaribia au kufikia kiwango cha kati cha nchi au sehemu zilizoendelea barani Asia.

Baada ya mpango huo kutolewa, watu wa Fuzhou walitekeleza mpango huo kwa juhudi kubwa, na malengo yote yaliyowekwa na Mpango wa Kimkakati wa “3820” yalifikiwa kwa wakati uliopangwa.