Nchi nyingi na mashirika ya kimataifa yameeleza kuunga mkono lengo la muungano la China na kupinga nchi za kigeni kuingilia kati mambo ya ndani ya China, ikiwa ni baada ya chaguzi mbili zilizofanyika Taiwan mwaka huu.
Nchi na mashirika hayo ya kimataifa zimesema, serikali kuu ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayowakilisha nchi nzima ya China, na Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya ardhi ya China.
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Kenya imetoa taarifa ikisema, Kenya inashikilia kanuni ya China moja, na kutaka kuheshimiwa kwa mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, na kutoingilia kati mambo ya ndani ya China.
Naye msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Meles Alem amesema, nchi hiyo inashikilia msimamo wake wa kanuni ya kuwepo kwa China moja.