Waziri mkuu wa Israel asisitiza kupinga kuanzishwa kwa taifa la Palestina
2024-01-22 08:42:44| criWaziri Mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu hivi karibuni alisema, hakutoa ahadi kwa Marekani kuhusu kukubali kuanzishwa kwa taifa la Palestina.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imekanusha kuwa Bw. Netanyahu aliwahi kutoa ahadi kwa rais wa Marekani Joe Biden kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa kuanzishwa kwa taifa la Palestina. Taarifa hiyo imesema, kwenye mazungumzo ya simu na rais Biden, Bw. Netayahu alisisitiza msimamo wake kwamba Israel lazima idumishe udhibiti wa usalama kwa pande zote kwenye Ukanda ya Gaza baada ya kuliangamiza kundi la Hamas, ili kuhakikisha Ukanda wa Gaza hautakuwa tishio tena kwa Israel.