Mkutano wa kilele wa 19 wa harakati za kutofungamana na upande wowote wafungwa mjini Kampala
2024-01-22 14:59:36| cri

Mkutano wa kilele wa 19 wa harakati za kutofungamana na upande wowote ulifungwa tarehe 20 Januari mjini Kampala, Uganda. “Azimio la Kampala” lilipitishwa kwenye mkutano huo na kutoa wito wa kushikilia utaratibu wa pande nyingi, kuimarisha ushawishi wa Harakati za kutofungamana na upande wowote kwenye mambo ya kimataifa, na kujitahidi kujenga dunia yenye amani, haki na ustawi.

“Azimio la Kampala” linasisitiza tena kanuni zilizowekwa mwaka 1961 kwenye mkutano wa Bandung wa mwaka 1955 na kuanzishwa kwa harakati hiyo, na kusisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano wa Kusini - Kusini na Kusini - Kaskazini, kuheshimu kwa pande zote sheria za kimataifa na kanuni za makubaliano ya kimataifa, kukabiliana kwa pamoja na tishio na changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

“Azimio la Kampala” pia limelaani vikali operesheni ya kijeshi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, na kutoa mara moja wito wa usimamishaji vita wa kibinadamu na wa kudumu.