Kilowati 100 za umeme zaanza kuingizwa kwenye gridi ya taifa
2024-01-22 23:21:06| cri

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania Dk Doto Biteko, amesema majaribio ya mtambo namba tisa kwenye mradi wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) yamekuwa na mafanikio makubwa na kilowati 100 zimeanza kuingizwa kwenye gridi ya taifa.

Dk Biteko ameeleza kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na wakandarasi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), akisema amefurahishwa na taarifa iliyotolewa na Makamu mkuu wa kampuni ya Elsewedy, Mhandisi Wael Hamdy kuhusu majaribio hayo.

Habari zinasema maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Arab Contractors ya Misri kwa sasa yamefikia asilimia 95.83.