Rais Xi Jinping ataka juhudi zote zifanywe kuwaokoa wahanga kufuatia maporomoko ya udongo kutokea mkoani Yunnan
2024-01-22 15:48:26| cri

Rais Xi Jinping wa China ameagiza juhudi zote zifanywe kuwatafuta na kuwaokoa watu ambao hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo kutokea Januari 22 katika kijiji cha Liangshui, wilaya ya Zhenxiong, mjini Zhaotong, mkoani Yunnan, ambayo yamefunika nyumba 18 na watu 47 hawajulikani walipo.

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Guoqing ameongoza kikosi kazi kwenda kwenye eneo la maafa, wizara ya maliasili na wizara ya menejimenti ya dharura zimeanzisha mwitiko wa dharua, na serikali ya mkoa wa Yunnan na mji wa Zhaotong zote zimeanza operesheni za uokoaji. Hivi sasa, kazi mbalimbali zinaendelea kwa utaratibu.