Waziri wa Mambo ya Nje ya China asema atashirikiana na Afrika katika kujenga dunia yenye usawa
2024-01-22 08:40:25| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amesema China iko tayari kushirikiana na Afrika katika kujenga dunia ya usawa na pande nyingi, na utandawazi wa uchumi unaonufaisha wote.

Wang Yi amesema hayo alipozungumza na wanahabari kuhusu ziara yake ya hivi karibuni katika nchi za Misri, Togo, Tunisia na Cote d’Ivoire za barani Afrika. Amesema, katika miaka ya karibuni, machafuko ya kisiasa na kiusalama katika kanda ya Afrika Magharibi, hususan, eneo la Sahel, kumeleta changamoto kwa amani, utulivu na maendeleo ya kikanda, na kusema China inatarajia kurejeshwa kwa amani na kutimiza utulivu na maendeleo katika kanda hiyo haraka iwezekanavyo.

Wang Yi ameongeza kuwa, ni muhimu kutatua tofauti za kisiasa kupitia mazungumzo na mashauriano.