Ajali ya moto yasababisha vifo vya watu wawili mjini Johannesburg, Afrika Kusini
2024-01-22 15:00:13| cri

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini tarehe 21 Januari viliripoti kuwa ajali ya moto imetokea kwenye jengo moja la ghorofa lililoko kwenye eneo kuu la biashara mjini Johannesburg, hadi sasa watu wawili wamethibitishwa kufariki na wengine wengi wamejeruhiwa, na watu takriban 150 wamepoteza makazi yao.

Meya wa Johannesburg Kabelo Gwamanda amesema hatua mbalimbali zinachukuliwa mara moja ili kutatua tatizo la makazi kwa walioathirika katika ajali hiyo.