Rais wa DRC aapishwa kuiongoza nchi hiyo kwa awamu nyingine
2024-01-22 08:36:43| cri

Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ameapishwa jumamosi iliyopita kuiongoza nchi hiyo kwa awamu yake ya pili ya miaka mitano.

Akizungumza baada ya kuapishwa, rais Tshisekedi aliahidi kuongeza ajira, kukuza uchumi wa viwanda na uchumi shirikishi, kuongeza uwezo wa ununuzi wa wakazi, na kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za msingi za maisha.

Pia rais Tshisekedi ameahidi kuimarisha ujenzi wa ulinzi wa taifa, na kupambana na makundi yenye silaha katika eneo la mashariki mwa DRC ili kufikia amani mapema.