Umoja wa Mataifa wazitaka Ethiopia na Somalia kuzungumza ili kutatua mgogoro kati yao
2024-01-22 10:22:17| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amezitaka Ethiopia na Somalia kufanya mazungumzo ili kusuluhisha mgogoro walio nao kuhusu mkataba wa baharini wa Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland.

Mvutano kati ya nchi hizo mbili umeongezeka tangu Ethiopia isiyo na bandari ilipofikia makubaliano na eneo la Somaliland kuhusu njia inayotafutwa sana Ethiopia ya kuingia baharini.

Eneo la Somaliland lilisema makubaliano hayo yangeifanya Ethiopia iitambue rasmi, lakini Ethiopia haikujibu lolote.

Somalia Alhamisi iliondoa uwezekano wa mazungumzo na Ethiopia isipokuwa kama makubaliano hayo yanafutwa, na kuapa kupambana kwa "njia zote za kisheria" kuyapinga.