Mjumbe maalum wa rais wa China ashiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa rais wa DRC
2024-01-22 08:38:52| CRI

Mjumbe maalum wa rais wa China, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bibi Shen Yueyue amehudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi iliyofanyika Jumamosi huko Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Jumapili, rais Tshisekedi alikutana na Bi. Shen Yueyue, ambapo alisema DRC inatilia maanani urafiki kati ya nchi hizo mbili, kushikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na inapenda kushirikiana na China kuimarisha ushirikiano katika nyanja muhimu ikiwemo sekta ya madini, ili kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika kiwango cha juu zaidi.  

Kwa upande wake, Bibi Shen amesema China inaunga mkono kithabiti maslahi makuu za pande hizo mbili, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, kukuza mawasiliano na ushirikiano chini ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afirka, ili kujenga uhusiano imara zaidi na wenye uhai mkubwa zaidi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na DRC.