Thamani ya biashara kati ya China na Zimbabwe yaongezeka kwa asilimia 29.9 mwaka 2023
2024-01-23 08:31:31| CRI

Thamani ya biashara kati ya China na Zimbabwe imefikia rekodi mpya ya dola za kimarekani bilioni 3.12 mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 29.9 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Katika taarifa yake kupitia mtandao wa X, Ubalozi wa China nchini Zimbabwe umesema biashara kati ya nchi hizo mbili imekuwa kidhahiri katika miaka ya karibuni, huku madini na tumbaku vikiongoza katika mauzo ya nje ya Zimbabwe nchini China.

Mwaka jana, bidhaa za kilimo kutoka Zimbabwe zilizouzwa nchini China ziliongezeka kwa kasi baada ya Zimbawe kuuza machungwa yake katika soko la China.