Mwakilishi maalumu wa rais wa China ashiriki kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Liberia
2024-01-23 08:35:22| cri



Mwakilishi maalumu wa rais wa China Bw. Bate’er alishiriki kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais Joseph Nyumah Boakai wa Liberia iliyofanyika jana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Monrovia.

Kabla ya hapo, rais mteule Boakai alikutana na Bw. Bate’er jumapili, ambapo Bw. Bate’er alimpa salamu kutoka kwa rais Xi Jinping, na kusema China inatilia maanani uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na inapenda kushirikiana na Liberia kuzidisha maelewano, kuimarisha ushirikiano na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande hizo mbili.