Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya kutembelea China
2024-01-23 18:57:41| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin ametangaza kuwa, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Dkt. Musalia Mudavadi atafanya ziara rasmi nchini China kuanzia tarehe 24 hadi 26 mwezi huu.