Zaidi ya watu 100 wajeruhiwa kufuatia tukio la kukanyagana katika shule ya sekondari nchini Cameroon
2024-01-23 08:32:11| CRI

Wanafunzi 106 wamejeruhiwa jana kufuatia tukio la kukanyagana katika shule ya sekondari ya juu ya Etoug-Ebe iliyopo Yaunde, mji mkuu wa Cameroon.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya ya Umma nchini humo, wanafunzi hao wanaendelea vizuri na timu ya huduma ya afya ya akili imeandaliwa kwa ajili ya wanafamilia.

Tukio hilo limetokea saa moja asubuhi kwa saa za huko wakati wanafunzi walipokuwa wakielekea madarasani baada ya maombi ya asubuhi.

Mkuu wa wilaya ya Mfoundi, Emmanuel Djikdent amesema, hakuna mwanafunzi aliyefariki katika tukio hilo.