China yapenda kushirikiana na washirika wa kimataifa kuunga mkono Comoros kudumisha utulivu wa jamii
2024-01-23 08:30:41| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China inapenda kushirikiana na washirika wa kimataifa kuunga mkono Comoros kudumisha utuliuvu wa jamii, ili kuchangia katika maendeleo ya amani ya nchi hiyo.

Akizungumza na wanahabari hapo jana, Wang Wenbin amesema, tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Comoros ilipotangaza kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo Azali Assoumani ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu tarehe 16 Januari, wafuasi wa upinzani wameandamana katika sehemu mbalimbali nchini humo, huku Marekani, Umoja wa Ulaya na Ufaransa zikitoa taarifa kuonesha mashaka juu ya matokeo ya uchaguzi huo.

Bw. Wang amesisitiza kuwa, uchaguzi wa rais ni mambo ya ndani ya Comoros, na kwamba China siku zote inashikilia kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kuhehsimu matakwa na chaguo la wananchi wa Comoros.