Israel yasema mazungumzo ya kusitisha mapigano kati yake na Palestina "yamepata maendeleo"
2024-01-23 08:29:12| cri

Shirika la Utangazaji la Israel limesema, mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas la Palestina "yamepata maendeleo."

Ripoti hiyo iliyotolewa jana imesema, maendeleo hayo yamepatikana baada ya kuona mabadiliko katika msimamo wa kundi la Hamas. Ripoti hiyo imemnukuu afisa wa usalama wa Israel akisema, masharti ya Israel katika mazungumzo hayo ni pamoja na kuwaachilia Waisraeli wote waliozuiliwa isipokuwa wanajeshi wa Israel, kusimamisha vita, kuwaondoa wanajeshi wa Israel katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza, na kuachiliwa huru kwa wafungwa wa usalama wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Israel ilitarajia kupokea majibu ya kundi la Hamas kwa masharti hayo jana, lakini kutokana na operesheni kubwa za jeshi la Israel huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, huenda jibu hilo likachelewa.