Mafuriko mjini Dar es Salaam yafanya barabara zisipitike
2024-01-23 14:02:24| cri

Nyumba kadhaa zimebomoka na barabara na madaraja kuharibiwa baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo la pwani ya Tanzania kwa muda wa siku mbili.

Baadhi ya barabara hazipitiki, hali iliyofanya baadhi ya watu kusimamisha shughuli zao za kila siku. Mvua hiyo kubwa iliyonyesha Jumamosi na Jumapili, imeathiri zaidi wilaya za Kinondoni na Ilala.

Daraja moja ambalo ni njia muhimu ya kuelekea katikati ya jiji halikuweza kupitika kutokana na mafuriko.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetahadharisha juu ya mvua kubwa kunyesha kwa muda wote wa mwezi huu, huku Rais wa Tanzania akiwataka watu kuondoka katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko.