Kituo cha wanahabari cha CMG nchini Nauru chazinduliwa
2024-01-24 13:46:34| cri

Baada ya kuidhinishwa na idara za serikali za nchi mbili, kituo cha wanahabari cha Shirika Kuu la Utangazaji la Taifa la China CMG huko Yaren, Nauru kimezinduliwa rasmi. Kituo hicho kimejengwa kwa msingi wa kituo cha ripoti cha Yaren kilichozinduliwa na kuendeshwa, ambacho kinasimamiwa na kituo kikuu cha Asia na Pasifiki cha CMG, kikiwa kituo cha 192 cha CMG kuzinduliwa katika nchi za nje.

China na Nauru leo zimesaini taarifa ya pamoja ya kurejesha uhusiano wa kibalozi. Waziri wa diplomasia na biashara wa serikali ya Nauru, Lionel Aingimea alipohojiwa na mwanahabari wa CMG, amesema kutambua Kanuni ya kuwepo kwa China Moja na kukatisha uhusiano wa kibalozi na mamlaka ya Taiwan ni uamuzi sahihi uliojadiliwa na kufanywa na serikali ya Nauru, ambao utaleta fursa mpya kwa maendeleo ya Nauru. Amekaribisha kituo cha wanahabari cha CMG huko Yaren kuripoti zaidi habari za Nauru kwa dunia nzima.