Watalii wanaokwenda Rwanda waongezeka karibu mara tatu ndani ya miaka miwili
2024-01-24 10:55:27| cri

Juhudi zilizowekwa katika kuondoa athari za janga la Covid-19 na kuongeza maradufu idadi ya ndege za Shirika la ndege la Rwanda kumefanya idadi ya watalii walioitembelea Rwanda iongezeke kwa mara tatu ndani ya miaka miwili.

Waziri Mkuu wa Rwanda Bw. Edouard Ngirente amesema idadi ya watalii waliofika Rwanda iliongezeka kutoka 521,000 mwaka 2021 hadi milioni 1.4 mwaka 2023.

Shirika la ndege la Rwanda lilianzisha safar za ndege baada ya janga la Covid-19 na kufungua njia mpya za kwenda maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na Paris, London, na Doha, hali iliyochangia ongezeko la idadi ya watalii kutoka 521,000 mwaka 2021 hadi watalii milioni 1.4 kufikia mwaka2023.