Sudan yapinga vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya taasisi za kiuchumi za nchi hiyo
2024-01-24 08:30:36| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imepinga vikali vikwazo visivyo halali vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya taasisi za kiuchumi za nchi hiyo.

Katika taarifa yake, Wizara hiyo imesema vikwazo hivyo havitasaidia kutimiza amani, na kuongeza kuwa, kulenga taasisi tatu zinazohusiana na Jeshi la Sudan ni jambo la kushangaza na kusikitisha.

Taarifa hiyo pia imesema, haki na wajibu wa Jeshi hilo kulinda nchi kunalilazimu jeshi hilo kutafuta vifaa vya ulinzi, na sheria zote zinahakikisha haki ya kujilinda.

Jumatatu wiki hii, Baraza la Umoja wa Ulaya liliweka vikwazo dhidi ya taasisi sita zinazohusiana na Jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF, ikiwemo kuzuia mali na kuzuia fedha ama rasilimali za kiuchumi, moja kwa moja ama kwa njia isiyo ya moja kwa moja.