Jumuiya ya kimataifa yaipongeza China kutokana na mafanikio yake ya kihistoria katika kulinda haki za binadamu
2024-01-24 10:59:27| cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa mjini Geneva, Balozi Chen Xu tarehe 23 Januari alihudhuria mjadala wa nne wa haki za binadamu katika Baraza la haki za binadamu la UM mjini Geneva, Uswisi.

Kwenye mjadala huo Balozi Chen alifafanua kwa pande zote njia ya maendeleo ya haki za binadamu ya China pamoja na mafanikio yake makubwa, akisisitiza kuwa China inashikilia kuheshimu na kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu uwe kazi muhimu katika utawala wa nchi. Kwenye mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa kichina, China inashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, na kulinda, kuhimiza na kuendeleza haki za binadamu katika hali ya usalama, maendeleo an ushirikiano.

Amesema zaidi ya nchi 120 zinaipongeza China kwa maendeleo iliyoyapata katika mambo ya haki za binadamu, na juhudi zake katika kuhimiza na kulinda haki za binadamu.