Watu 6 wauawa katika risasi za basi nchini Ghana
2024-01-24 08:31:44| criWatu sita wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na kikundi cha watu wasiojulikana wenye silaha dhidi ya basi katika mkoa wa Upper East nchini Ghana. 

Mtendaji mkuu wa mji wa Bawku Bw. Hamza Amadu amesema, shambulio hilo limetokea jumatatu wakati abiria hao walipokuwa safarini kutoka Bawku kuelekea kwenye soko kubwa lililoko katika mji wa jirani.

Amadu alisema waliokufa ni pamoja na watu wawili na wanawake wanne, na majeruhi wanapokea matibabu katika hospitali mbili za karibu.