China yapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi na nchi nyingine
2024-01-24 08:31:12| cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali jana ilitoa waraka mweupe kuhusu "Mfumo na Utekelezaji wa Sheria ya Kupambana na Ugaidi wa China". Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Wang Wenbin amesema, China inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine katika mapambano dhidi ya ugaidi, kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani, kuhimiza maendeleo mazuri ya mapambano hayo, na kudumisha amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.

Bw. Wang amesema, waraka huo unaeleza kwa kina na kwa utaratibu mfumo na utekelezaji wa sheria ya mapambano ya China dhidi ya ugaidi, ikiwa ni pamoja na viwango vya utambuzi na kanuni za adhabu kwa vitendo haramu na uhalifu wa vitendo vya kigaidi, na kanuni za utekelezaji wa madaraka katika kazi ya mapambano na kulinda haki za binadamu kwa kufuata sheria.