Naibu Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na Rais Samia
2024-01-24 10:58:16| cri

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Liu Guozhong mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Bw. Liu yuko nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu ambapo anatarajiwa kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na eneo la makaburi ya wataalam wa China waliopoteza maisha yao wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA.