Nchi zinazotumia Ziwa Victoria zakutana kujadili uchafuzi katika Ziwa hilo
2024-01-24 08:29:58| CRI

Wawakilishi kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi wamekutana jijini Dar es Salaam, Tanzania, kwa lengo la kujadili uchafuzi unaosababishwa na shughuli za kibinadamu katika Ziwa Victoria.

Msimamizi wa mradi wa maendeleo katika Tume ya Bonde la Ziwa Victoria, Hilda Luoga amesema katika mkutano huo kuwa, mradi wenye thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani unaolenga kurejesha hadhi ya Ziwa Victoria unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Amesema mradi huo utakaotekelezwa chini ya Tume hiyo kwa miaka kumi, unahusisha kudhibiti taka ngumu, usafi na mifumo ya majitaka inayochafua Ziwa Victoria, na kuonya kuwa, Ziwa hilo linalotumia na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, linakabiliwa na uchafuzi mkubwa unaotokana na shughuli za kibinadamu.