Tanzania kuwa na mfumuko wa chini kabisa wa bei Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa 2024
2024-01-24 22:50:30| cri

Tanzania itaweka rekodi ya kuwa na kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa mwaka 2024.

Makadirio ya mwelekeo wa Uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 yaliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), yanaonesha kuwa eneo la Afrika Mashariki linaelekea katika ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.9 mwaka huu, lakini Tanzania itakuwa katika nafasi ya mbele kwa kuwa na mfumuko wa chini wa bei.

Tanzania inafuatiwa na Uganda na Kenya, ambazo viwango vya mfumuko wake wa bei vinakadiriwa kuwa asilimia 5 na 6.5, chini kutoka asilimia 5.6 na 7.5 mtawalia.