Nchi wanachama wa EAC waridhia sera ya kuhama kwa nguvukazi
2024-01-25 08:30:48| CRI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameridhia sera ya Jumuiya hiyo na mfumo wa kisheria unaosimamia uhamaji wa nguvukazi.

Taarifa iliyotolewa jana katika makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha, Tanzania, lengo la sera hiyo ni kutetea ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji, kuimarisha usimamizi wa uhamaji wa nguvukazi, na kutumia vizuri faida zinazotokana na uhamaji wa nguvukazi.

Hatua hiyo ilitangazwa wakati wa mkutano wa wakurugenzi wa kazi na ajira wa nchi wanachama wa EAC uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi, jumanne wiki hii.

Sera hiyo itaanza kutekelezwa mwaka 2025 hadi 2030 na inalenga maeneo muhimi kama usimamizi wa uhamaji wa nguvukazi, masikilizano ya sera za uhamaji wa nguvukazi, na kutambua kwa pamoja sifa za kitaaluma na elimu.