Mahakama Kuu ya Comoros yatangaza rais Azali ameshinda katika uchaguzi mkuu
2024-01-25 09:29:41| cri


Mahakama Kuu ya Comoros jana imetangaza kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo Azali Assoumani amepata zaidi ya nusu ya kura kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni, na kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

Mahakama hiyo imesema rais Azali amepata asilimia 57.02 ya kura, na kwa mujibu wa katiba ya Comoros, mgombea aliyepata kura zaidi ya nusu kwenye duru ya kwanza ya upigaji kura atakuwa ameshinda nafasi ya urais.