Rwanda yafanya juhudi kupata maendeleo katika sekta ya akili bandia (AI)
2024-01-25 11:01:31| cri

Serikali ya Rwanda imeongeza kasi ya kuendeleza sekta ya akili bandia (AI), na kuweka mipango kadhaa ya kuwa kituo muhimu cha teknolojia ya akili bandia barani Afrika.

Hatua hizo ni pamoja na kuwa mwenyeji wa kituo pekee cha mapinduzi ya nne ya viwanda barani Afrika, kuanzisha sera ya taifa ya maendeleo ya teknolojia ya akili bandia, kuanzisha sera ya Ulinzi wa Data binafsi, kukaribisha uandaaji wa matukio yanayolenga eneo la akili bandia, kuwa mwenyeji wa kampuni ya BioNTech barani Afrika, kuwa mwenyeji wa kituo cha Norrsken House mjini Kigali ambacho ni kituo kikubwa zaidi cha ujasiriamali barani Afrika, na kukaribisha kuwa makao makuu ya Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon barani Afrika. Chuo kikuu hiki kinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya elimu na utafiti wa kiwango cha juu katika kuandaa taifa kwa ajili ya teknolojia za Akili bandia.