Marais wa China na Uzbekistan wafanya mazungumzo
2024-01-25 08:09:36| CRI

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev jumatano mjini Beijing, ambapo viongozi hao wawili wametangaza kuwa, nchi hizo mbili zimeamua kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati katika pande zote, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Uzbekistan yenye mustakabali wa pamoja.

Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesema, pande hizo mbili zinatakiwa kujenga msingi imara wa jumuiya ya China na Uzbekistan yenye mustakabali wa pamoja kwa kufuata kanuni ya kuaminiana kisiasa katika kiwango cha juu, na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa pande zote mbili kwa njia ya ujenzi wenye sifa bora wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Kwa upande wa rais Mirziyoyev amesema, Uzbekistan inapenda kuimarisha kuaminiana kisiasa na China na kupanua ushirikiano kwa pande zote, ili kujenga kwa kiwango cha juu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.