Watu 9 wauawa kwa kuchomwa moto katika shambulizi dhidi ya kituo cha mafunzo cha Umoja wa Mataifa huko Gaza
2024-01-25 08:28:56| cri

Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina katika kanda ya Mashariki ya Karibu la Umoja wa Mataifa (UNRWA) Bw. Thomas White jana amesema, watu 9 wameuawa na wengine 75 kujeruhiwa baada ya shambulio dhidi ya kituo cha mafunzo cha UNRWA huko Khan Younis, mji ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza, lililosababisha moto mkubwa.

Bw. White alisema, kulikuwa na maelfu ya watu wasio na makazi wanaoishi katika kituo hicho wakati kiliposhambuliwa, na kwamba timu za misaada za UNRWA na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Ukanda wa Gaza zinajitahidi kufikia eneo la tukio.