Fedha zinazotumwa kwenye eneo la Afrika Mashariki kutoka nje zaongezeka na kufikia rekodi ya dola za Marekani bilioni 9.3
2024-01-25 11:00:43| cri

Benki ya Dunia imesema utumaji wa pesa sasa ni mojawapo ya vyanzo vikubwa vya fedha katika eneo la Afrika Mashariki, na pesa kutoka nje zilizotumwa kwenye eneo hilo kwa mwaka 2022 zimeongezeka na kuweka rekodi ya dola za Kimarekani bilioni 9.3, licha ya gharama kubwa za utumaji wa fedha hizo.

Mwaka 2021, utumaji wa pesa kutoka kwa diaspora ya wakenya ulifikia thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.718, fedha kutoka diaspora ya waganda zilifikia dola milioni 599.3, kutoka diaspora ya watanzania zilikuwa dola za Marekani milioni 569.5, na kutoka diaspora ya wanyarwanda ilikuwa dola za Kimarekani milioni 246. Wachambuzi wa biashara katika eneo la Afrika Mashariki wanasema fedha zinazotumwa na diaspora zimekuwa ni chanzo kikubwa zaidi cha fedha kutoka nje ya eneo hilo.