Mahakama kuu ya Comoro yatangaza Azali Assoumani amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo
2024-01-25 11:08:25| cri

Mahakama kuu ya Comoro jana ilitangaza kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo Azali Assoumani amechaguliwa tena kuendelea na madaraka yake baada ya kupata zaidi ya nusu ya kura katika upigaji kura wa duru ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Comoro, mgombea anayepata kura zaidi ya nusu katika duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu anatangazwa kuwa mshindi.