Ripoti ya UM yasema vurugu za magenge nchini Haiti zimesababisha vifo zaidi ya 4,700 mwaka 2023
2024-01-25 11:07:50| cri

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imeonyesha kuwa watu 4,789 wamekufa kutokana na vurugu za magenge nchini Haiti katika mwaka 2023 huku matukio ya mauaji nchini humo yakiongezeka kwa asilimia 119.4 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema vurugu hizo zimeathiri maisha ya watu wa Haiti ambapo vitendo hivyo vya ukatili vinaendelea bila hatua kuchukuliwa.

Ripoti hiyo pia imesema sasa magenge yamezidisha mashambulizi dhidi ya polisi, vituo zaidi ya 45 vya polisi kati ya 412 nchini Haiti viliteketezwa kwa moto katika mwaka 2023.