Msomi wa Tanzania: China ni rafiki wa kweli wa Afrika
2024-01-26 14:50:42| CRI

Mwaka huu wa 2024, China itaandaa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ambapo viongozi wa China na Afrika watakutana tena nchini China baada ya Mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika mwaka 2018 hapa Beijing. Mkurugenzi wa Kituo cha Sera ya Kimataifa-Afrika (CIP-Africa) Bw. Omar Mjenga amepongeza michango muhimu ya FOCAC, na kuona kuwa mipango na ruwaza ya FOCAC vinakaribishwa na kupokelewa vizuri na nchi za Afrika. 

Bw. Omar Mjenga amesema, katika miaka ya karibuni chini ya mfumo wa FOCAC, China imetangaza kwa nyakati tofauti “Mipango Kumi ya Ushirikiano kwa Afrika”, pamoja na “Hatua Nane” na “Miradi Tisa”, ambapo ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika umezidi kuimarika. Ametolea mfano kuwa China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka 14 mfululizo, bidhaa zilizotengenezwa China zinajulikana kote barani Afrika, na watu wa Tanzania, kuanzia watoto hadi wazee, wote wanafahamu chapa nyingi za China. Wakati huohuo, kinachowafurahisha watu wa Afrika ni kwamba, China pia imefungua soko lake kwa bidhaa za Afrika, na sasa bidhaa nyingi za Afrika zimekaribishwa sana na wateja wa China. Mbali na hayo, China pia inajitahidi kutoa uzoefu na matunda ya maendeleo yake ya sayansi na teknolojia kwa Afrika na kuhamisha teknolojia zake kwa nchi za Afrika. 


Bw. Mjenga anaona, wanapokabiliana na njama za nchi za Magharibi za kuupaka matope ushirikiano kati ya Afrika na China, wanayotaka kusema watu wa Afrika ni kwamba hawataki kuambiwa jinsi ya kuchagua wenzi, na wanajua wazi nani ni rafiki wa kweli. Baadhi ya nchi za Magharibi zimekuwa zikijaribu kukwamisha jitihadi zote zinazofanywa na China barani Afrika, lakini nchi za Afrika na watu wao wanajua kuwa China ni rafiki wanamuyehitaji na pia ni rafiki mkubwa wa kweli.