Rais wa mpito wa Burkina Faso atangaza sheria mpya kufuta hadhi ya lugha rasmi ya Kifaransa
2024-01-26 10:36:53| cri

Rais wa mpito wa Burkina Faso Ibrahim Traore ametangaza sheria ya kurekebisha katiba inayotoa fursa ya kushusha hadhi ya Kifaransa kutoka lugha rasmi hadi lugha ya kazi, sawasawa na Kiingereza. Licha ya hayo, imefuta Baraza la Kiuchumi na Kijamii (CES), na kukabidhi majukumu yao kwa Baraza la Kitaifa la Jumuiya lililoundwa upya. Mahakama Kuu pia imefutwa na mamlaka yake kuhamishiwa kwa Mahakama ya Rufaa ya Ouagadougou.