Tanzania, Cuba zasaini makubaliano kuboresha sekta ya afya, elimu
2024-01-26 10:21:47| cri

Serikali ya Tanzania na Cuba zimesaini hati mbili za makubaliano na kukubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano wao katika sekta za afya, elimu, kilimo na kuendelea kuboresha uhusiano wa siasa na uchumi.

Hati hizo ni makubaliano ya Chuo Cha Artemisia Dius Gonzales Cha Cuba na Chuo Cha Kilimo Cha Sokoine, na hati ya makubaliano kati ya Kituo cha tiba cha Cuba (CECMED) na Mamlaka ya Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), katika kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya kiwanda cha dawa za malaria kilichopo Kibaha na kuzalisha dawa nyingi za binadamu na za kuua wadudu.