Watu 10 wauawa kwenye shambulio katikati ya Nigeria
2024-01-26 09:41:03| criWatu 10 wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye shambulio lililotokea katikati ya wiki hii katika jimbo la Plateau nchini Nigeria.

Msemaji wa polisi wa jimbo hilo Alfred Alabo jana amesema, washambuliaji hao walishambulia jamii ya Kwashalek huko Mangu Jumanne na Jumatano, na kubomoa takriban nyuma 10.

Shambulio hilo la hivi karibuni linafuatia mashambulio mfululizo katika mkoa huo yaliyotokea wakati wa msimu wa sikukuu ya Krismas na kusababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa.

Alabo amesema sababu ya shambulio hilo bado haijulikani.