Rais Museveni asema Uchumi wa Uganda bado unavutia uwekezaji
2024-01-26 23:20:58| cri

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema Serikali itakamilisha mkakati wa "kuongeza pato la Taifa la Uganda mara kumi ndani ya muongo mmoja", na kusema katika hatua hiyo uwekezaji kwenye maendeleo ya raslimali watu "utaendelea kupewa kipaumbele, ikiwa ni pamoja na kushughulikia utawala mbovu na ufujaji wa raslimali za umma.

Rais Museveni pia amesema serikali itahimiza maendeleo ya viwanda, na kutaja baadhi ya hatua za kuhimiza uwekezaji kwenye viwanda kuwa ni pamoja na kuunga mkono uendelezaji wa bustani za viwanda.

Pia amesema mamlaka ya Uwekezaji ya Uganda imepata maili 12 za mraba zaidi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda, zilizotolewa na serikali za mitaa katika kanda 18 nchini Uganda.