China yapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa
2024-01-26 08:27:50| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema jana kuwa, China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa chini ya mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kujenga "Ukanda wa maendeleo" na "barabara zenye furaha" zinazonufaisha nchi zote, kukuza maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja, na kutoa mchango mkubwa katika mambo ya kisasa duniani.

Kauli hiyo imetokana na ripoti iliyochapishwa katika jarida la "Sera za Kidiplomasia" la Marekani ambayo inasema kuwa mgogoro wa sasa wa Bahari Nyekundu unaonyesha kuwa mpango wa China wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni muhimu na ndio mwongozo ambao kila nchi inahitaji katika zama zilizojaa hali ya sintofahamu na ghasia.