Wizara ya mambo ya nje ya Iraq yasema Iraq itazungumza na Marekani kuhusu kuondoa vikosi vya muungano wa kimataifa nchini Iraq
2024-01-26 10:44:31| cri

Taarifa iliyotolewa tarehe 25 na wizara ya mambo ya nje ya Iraq imesema tangu mwezi Agosti mwaka jana serikali ya Iraq imefanya mazungumzo ya duru nyingi na Marekani kuamua kuunda kamati moja ya kijeshi ya ngazi ya juu ili kutathmini hali ya usalama ya sasa nchini Iraq, na hatari ya tishio kutoka makundi yenye msimamo mkali, na kuimarisha uwezo wa jeshi lake.

Taarifa imesema chini ya mfumo wa kamati hiyo, Iraq na Marekani zitaweka ratiba ya kuhakikisha muda wa kuwepo kwa vikosi vya muungano wa kimataifa nchini Iraq, na kupunguza idadi ya wanajeshi wa muungano huo nchini humo hatua kwa hatua, na hatimaye kuhitimisha misheni ya kijeshi ya muungano huo dhidi ya makundi yenye msimamo mkali, na badala yake kuweka mikataba kati ya Iraq na nchi husika.