Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Kenya wafanya mazungumzo
2024-01-26 08:28:24| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi hapa Beijing.

Katika mazungumzo yao, mawaziri hao wamekubailiana kufuata makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, na kuhimiza ujenzi wa Jumuia ya China ya Kenya yenye mustakabali wa pamoja.

Katika mazungumzo hayo Bw. Wang Yi amesema, katika miaka 60 iliyopita tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Kenya uanzishwe, nchi hizo mbili zimekuwa zikielewana na kuungana mkono, na miradi mbalimbali ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ikiwemo reli ya SGR imechangia maendeleo ya uchumi nchini Kenya. Pia amesisitiza kuwa China inaiunga mkono Kenya kujiendeleza, na kupenda kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kupanda katika ngazi ya juu zaidi.

Kwa upande wake Bw. Mudavadi amesisitiza kuwa Kenya itashikilia kithabiti kuwepo kwa China moja, na kutarajia kuimarisha ushirikiano wa karibu zaidi na China.